TEKNOLOJIA NI NJEMA
Tumeipenda tovuti Makazini manyumbani
Kufanyia utafiti Hata kwetu masomoni
Ndio wa mgongo uti Kiuchumi kwetu nchini
Teknolojia ni njema Ikitumiwa ipasavvyo
Tukiwashe kiberiti Tujitie mpangoni
Tuikaze na boriti Wakosao tumaini
Tuzisome ripoti Toka mtandaoni
Teknolojia ni njema Ikitumiwa ipasavvyo
Jamani tusiketi Eti ni ya uzunguni
Tulivalie kabuti Tuelekee mwezini
Tusijifunge kwa neti Tujikaze kisabuni
Teknolojia ni njema Ikitumiwa ipasavvyo
No comments:
Post a Comment