Thursday, June 9, 2011

WENZANGU JIKONTROLINI


WENZANGU JIKONTROLINI

Najitupa stejini                       Nieleze ya moyoni
Siseme sikuelezeni                 Hata nikifahamuni
Matatizo duniani                     Taingia ta mwilini
Wenzangu jikontrolini             Tusihame duniani

Siseme hayasemwi                Ya ugonjwa wa ukimwi
Umetajwa kama zimwi            Ambalo halizimwi
‘ti maisha hujikimwi                Ukiupata ukimwi
Wenzangu jikontrolini              Tusihame duniani

Tangu darasa la pili                 Nimejifunza ukweli
Esitiae ni kali                          Ingawa bakteriali
Pia kuna  ya fungal                  Denjerasi vairali
Wenzangu jikontrolini              Tusihame duniani

Kama wewe ni msomu            Basi tumia kondomu
Sijigambe kwazo hamu           Kutafuna nyamu nyamu
Utajukuta na sumu                  Uanze kujilaumu
Wenzangu jikontrolini              Tusihame duniani

PWEZA


PWEZA

Pweza huyu ni hatari              Kwa hekima katabiri
Nishindwalo hafikiri                Na huishi kifahari
Karibuni yalojiri                      Waloshinda wana heri
Waloshindwa wana mori         Asemalo si la siri

Nakuomba wewe pweza         Sinitabirie giza
Chakulacho ukimeza              Siwezi kukupuuza
Kijaribu nichokoza                  Pweza tanichukiza
Uongo ukieneza                     Dunia takufukuza

Pweza kwangu mi sitaki         Utabiri ulo feki
Kwangu mi nataka haki          Usije nipaka chaki
Ukicheza mi sicheki               Nitakuchoma mkuki
Kijaribu nimiliki                      N’takuhepa kipikipiki

MWANAMKE MCHESHI


MWANAMKE MCHESHI

Mwanamke mcheshi               Hana la kuogopa
Hata kiona moshi                    Mbele atajitupa
Hapendi la uzushi                    Kimgusa utalipa
Sijigambe na ubishi                 Tajikuta ukihepa

Nyumbani anamoishi               Siingie kwayo pupa
Takutoa kama jeshi                 Hatashindwa kukuchapa
Kama hilo halitoshi                 Takuweka kwenye pipa
Tajikuta ukiwishi                     Kugeuka uwe papa

Mara kadha ye hakeshi           Kuitisha kadha chupa
Ni ngumu kumshawishi            Pesa zake kuzikopa
Mwanamme hamlishi              Akitaka tanenepa
Maishaye anapushi                  Utasema ni msupa

Monday, May 23, 2011

SIKU YA KIAMA


SIKU YA KIAMA
Ya kiama katabiri                       Dunia ‘ta tamatika
Kwa hamu tukasubiri                 Siku hiyo kihakika
Wengine wakahubiri                  Bwana yesu atashuka
Sijitupe kwa kaburi                   Wenzako watateseka

Siku hiyo ni ya siri                     La kwako ni kuokoka
Ombea wenzako heri                Wasije wakateseka
Usiisambaze habari                   Eti mwisho keshafika
Sijitupe kwa kaburi                   Wenzako watateseka

Siliuze lako gari                         Matope utajipaka
Utapandwa nayo mori               Wenzako wakikucheka
Siogope  kufikiri                        Majukumu kujitwika
Sijitupe kwa kaburi                   Wenzako watateseka

Thursday, May 12, 2011

MVUA HII WANITISHA


MVUA HII WANITISHA
Kibaridi chaniweza                 Ni mvua ilonyesha
Sitaki kufukuza                       Hata kama wanitisha
Tangu nane wajikaza               Ni jioni bado tosha
Taka hadi kuwe giza               Ndipo hasa jikomesha

Matope wayaongeza               Na viatu wazeesha
Ni furaha wanitoza                 Ta ingawa wanilisha
Wako mwenendo punguza     Matembezi kuyapisha
Nakuomba we tuliza               Ndiposa usije chosha

Mi sitaki nije cheza                 Ukulima Wadumisha
Sitaki njaa kujilaza                  Sababu kukufurusha  
Naomba kunisikiza                  Hali hewa imarisha
Usije ukaniliza                        Cha ukoka kunivisha