SIKU YA KIAMA
Ya kiama katabiri Dunia ‘ta tamatika
Kwa hamu tukasubiri Siku hiyo kihakika
Wengine wakahubiri Bwana yesu atashuka
Sijitupe kwa kaburi Wenzako watateseka
Siku hiyo ni ya siri La kwako ni kuokoka
Ombea wenzako heri Wasije wakateseka
Usiisambaze habari Eti mwisho keshafika
Sijitupe kwa kaburi Wenzako watateseka
Siliuze lako gari Matope utajipaka
Utapandwa nayo mori Wenzako wakikucheka
Siogope kufikiri Majukumu kujitwika
Sijitupe kwa kaburi Wenzako watateseka
No comments:
Post a Comment