PWEZA
Pweza huyu ni hatari Kwa hekima katabiri
Nishindwalo hafikiri Na huishi kifahari
Karibuni yalojiri Waloshinda wana heri
Waloshindwa wana mori Asemalo si la siri
Nakuomba wewe pweza Sinitabirie giza
Chakulacho ukimeza Siwezi kukupuuza
Kijaribu nichokoza Pweza tanichukiza
Uongo ukieneza Dunia takufukuza
Pweza kwangu mi sitaki Utabiri ulo feki
Kwangu mi nataka haki Usije nipaka chaki
Ukicheza mi sicheki Nitakuchoma mkuki
Kijaribu nimiliki N’takuhepa kipikipiki
No comments:
Post a Comment