MWANAMKE MCHESHI
Mwanamke mcheshi Hana la kuogopa
Hata kiona moshi Mbele atajitupa
Hapendi la uzushi Kimgusa utalipa
Sijigambe na ubishi Tajikuta ukihepa
Nyumbani anamoishi Siingie kwayo pupa
Takutoa kama jeshi Hatashindwa kukuchapa
Kama hilo halitoshi Takuweka kwenye pipa
Tajikuta ukiwishi Kugeuka uwe papa
Mara kadha ye hakeshi Kuitisha kadha chupa
Ni ngumu kumshawishi Pesa zake kuzikopa
Mwanamme hamlishi Akitaka tanenepa
Maishaye anapushi Utasema ni msupa
No comments:
Post a Comment